Friday, 18 August 2017

FURAHA ZATAWALA UJIO WA WANAFUNZI

Kilimanjaro. Furaha imetawala ujio wa watoto watatu wa Shule ya Lucky Vicent  waliowasili leo Ijumaa, Agosti 18 wakitokea nchini Marekani kwenye matibabu baada ya kupata ajali Mei mwaka huu.

Wazazi na ndugu waliruhusiwa kuingia ndani ya ndege hiyo kuwapokea watoto wao ambao wamepata nafuu kwa kiasi kikubwa.

Wilson Tarimo alikuwa wa kwanza kushuka katika ndege akiambatana na mdogo wake aliyeingia katika ndege kwa ajili ya kumpokea.

Baada ya hapo aliyefuatia ni Saidia  Awadhi pili akifuatana na Doreen Mshana  kushuka katika ndege hiyo iliyokuwa na wajumbe 16 ambao waliambatana na watoto hao.

Labels:

0 Comments:

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home