Monday, 21 August 2017

"Rumble in the Jungle". pambano lenye historia ya boxing


Rumble in the Jungle
"Rumble in the Jungle  ni mechi ya kihistoria  ambayo ilifanyika Oktoba 30, 1974 katika Uwanja wa Mei 20 huko Kinshasa, Zaire (sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo). Ilikuwa ni kati ya Bingwa wa Dunia wa Uzito wa juu George Foreman dhidi ya bingwa wa zamani na mshindi wa # 1 Muhammad Ali, aliyekuwa mpiganaji bora wa muda wote, baada ya Floyd Patterson.
Tukio hili lilikuwa ni mradi wa kwanza wa Don King kama mtetezi (promoter) wa ndondi.Don King aliweza kuwapata mabondia wote Ali na Foreman na kukubaliana kupambana ikiwa angeweza kuwalipa dola za kimarekani $ 5,000,000 kwa kila mmoja. Hata hivyo, King hakuwa na fedha, kwa hiyo alianza kutafuta nchi ya nje ili kudhamini tukio hilo. Rais wa Zaire  Flamboyant, Mobutu Sese Seko, aliomba pambano hilo lifanyike katika  nchi hiyo,
Mpambano ulionyeshwa kwenye televisheni iliyofungwa ya karibu na maeneo 450 nchini Marekani na Canada na ulionekana katika nchi karibu 100 duniani kote. Mapigano yalipangwa kuanza saa 10:00 alfajiri mjini Zaire ili kuwezesha kuhudhuriwa na watazamaji huko Marekani.

The Rumble

George Foreman vs Muhammad Ali

Promoter: Don King

Refari: Zach Clayton

Majaji:
  Nourridine Adalla
James Taylor

Wahuzuriaji: 60,000

Mataji
World Boxing Council Heavyweight Title (3rd defense by Foreman)

World Boxing Association Heavyweight Title (3rd defense by Foreman).

George Foreman  alikuwa na uzito wa  220 pounds
Muhammad Ali alikuwa na uzito wa 216½ pounds

Pambano lilianza kwa kasi na Foreman alianza kwa kushambulia sana na Ali alianza kwa kuzuia sana  na alikuwa anatumia staili yake ya "Rope-a- Dope" inayo maanisha  “Get away from the ropes,”  staili ambayo aliitungia msemo wa "I fly like a butterfly and I sting like a bee" staili ilimchosha sana Foreman adi kufika mzunguko wa 8 (8round) Foreman alikuwa amechoka sana apo Ali ndipo Ali aliporusha ngumi za kuunganika (combination) ambazo ni left hook akamalizia na right straight punch on face, Foreman akaenda chini refari Zach Clayton akamuhesabia  Foreman ambae alishindwa kuenderea na mpambano na kumtangaza "The Greatest" Muhammad Ali kuwa ndio mshindi wa Rumble in the Jungle.

Ali akiwa amemdondosha Foreman

 
Promoter Don King

 
Foreman akimshambulia Ali 

Foreman akimshambulia Ali
Foreman akiwa chini raundi ya nane kati ya raundi 15.

Labels:

0 Comments:

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home