Sunday, 3 September 2017

AMATEUR BOXING

Amateur boxing ( ngumi za lidhaa) hii ni njia ya mabingwa wote wa boxing unaowajua duniani kote kila professional boxer ameanzia kwenye amateur boxing, hii ni tofauti na
ndondi za kulipwa, hii hufanyika katika ngazi ya Michezo ya Olimpiki,
Michezo ya Pan American na Michezo ya Jumuiya ya Madola, pamoja na vyama vingi vya ngumi dunia.
Mapambano  ya ndondi ya amateur ni ya muda mfupi, yenye round tatu za dakika tatu kwa wanaume, na round nne za dakika mbili kwa wanawake, na dakika moja ya kupumzika kila baada ya round moja. Aina hii ya ngumi alama zinahesabiwa kwa kuangalia idadi ya ngumi alizompiga mpinzani wake na sio uzito wa ngumi anazo mpiga mpinzani wake, Pia, aina hii ya ndondi inaruhusu bondia kupambana kila baada ya muda mfupi tofauti na ndondi za kulipwa ambapo mabondia wanaweza kupambana baada ya miezi mingi. Hii ndio amateur boxing kwa ufupi.

Vifaa anavya vaa bondia wa Amateur;-

>Gum shield.

>Gloves zisizo umiza kama zile za ngumi za kulipwa.

>Kaushi, (mabondia wa Amateur hawapigani vifua wazi)

>Head protector (kofia ya kichwani) (katika vipindi  baadhi)

>N.K.

Labels:

0 Comments:

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home