Saturday, 9 September 2017

Treni ya Starehe ilioundwa India


Treni ya Tejas Express imeanza kazi na husafiri kati ya Mumbai na jimbo la kitalii Goa.

Tejas Express ina mabehewa yalio na viti vya starehena burudani ikiwemo filamu za Bollywood zinazoonyeshwa.

Treni hiyo pia ina mtandao kupitia wi-fi, michezo ya kompyuta na pia mtu anaweza kusikiliza matangazo na muziki.

Treni ya Tejas Express husafiri kwa saa nane na nusu kufika Goa kutoka Mumbai, hii ikiwa na kasi zaidi kidogo ikilinganishwana na treni nyingine.

Treni hiyo ina milango ya kufunguka wenyewe, otomatiki ni ya kwanza nchini India. Inaweza kwenda kwa mwendo kasi wa kilomita 200 kwa saa, lakini kuna udhibiti wa kasi wa treni nchini.

Inatarajiwa kuhudumu mara tano kwa wiki, kando na wakati wa msimu wa upepo mkali ambako itakuwa ikihudumu mara tatu kwa wiki.

Kuna mashine za chakula na vinywaji kama chai na kahawa ndani ya treni.
"Ni kama huduma ya ndege," abiria mmoja ameliamba shirika la habari AFP. "Nadhani hii treni ni fikra nzuri."

Tiketi za kawaida huuzwa $18; huku za kiwango cha juu ni rupi 2,590
Iwapo treni hiyo itapata umaarufu maafisa wanapanga kupanua huduma wakianza na jimbo jirani la Gujarat , ka mujibu wa taarifa.

appeared first on: http://www.bbc.com/swahili/habari-40043676

Labels:

0 Comments:

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home